KADA WA CHADEMA ATIWA MBARONI KWA KOSA LA KUM MWAGIA TINDIKALI NDUGU MUSA WAKATI WA UCHAGUZI WA IGUNGA

MUSA TESHA  BAADA  YA  KUMWAGIWA  TINDIKALI
------------------
Kada maarufu wa CHADEMA Shinyanga mjini,Bwana Oscar Kaijage,Jumamosi alikamatwa na askari polisi na kuzuiwa kituo cha kati na jana Jumatatu alisafirishwa kwenda Tabora na kukabidhiwa kwa askari wa huko.

Sababu kuu ya kukamatwa,ni kuhusishwa na tukio la kumwagiwa tindikali Bwana Musa Tesha 9 Sept,2011 huko Igunga kwenye kampeni za uchaguzi mdogo wa Mbunge ambapo mgombea wa CCM bwana Peter Kafumu alimshinda mgombea wa CHADEMA bwana Joseph Kashinde.

Bwana Oscar alifuatwa dukani kwake stand ya mabasi ya  Shinyanga mjini mnamo saa 9 mchana  na askari nane ambao hawakuvaa sare.

Baada ya mazungumzo ya muda mfupi askari hao waliwaomba majirani wa duka hilo wasogee  ili wawe mashuhuda  wakati wanampekua.

Hata hivyo,polisi  hao hawakukuta kitu chochote walichokihitaji na kuamua kuondoka naye kwenda kumpekua nyumbani kwake ambako nako pia hawakuambulia kitu.


Taarifa iliyopatikana  jana  mchana  kutoka ofisi ya RPC shinyanga ni kuwa Oscar amepelekwa Tabora kwenda kufunguliwa mashitaka.

Posted by Bigie on 3:46 PM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.