MTAZAMO: OMBA OMBA WATAFUTIWE SULUHISHO LA KUDUMU

Ndugu watanzania wenzangu, Inasikitisha  sana  kuwaona ombaomba wengi katika  maeneo  mengi  ya  dodoma na  eneo la Ubungo mkoani Dar es salaam na maeneo mengine ya mikoani wakiwa katika maeneo hayo kila siku. ..


Pamoja na kuwasaidia fedha kidogo msaada huo hautoshi kuwaondoa pale walipo kutokana na hali zao za kutokuwa na uwezo wa kufanya kazi za kutumia nguvu.

Wakati serikali yetu ikipitisha bajeti zenye kutumia fedha nyingi kwa kulipana posho na mishahara minono kwa watumishi wa ngazi za juu hasa wabunge na mawaziri inatakiwa pia kuwakumbuka walemavu wale wasio na msaada wowote wa kuwafanya waishi kama watanzania wegine kwa kuwaanzishia vituo maalumu ambapo watapata huduma na kutunzwa ..

 
Naomba ndugu wananchi na wabunge tuishinikize serikali ili iweze kulifanyia kazi swala hili kwani hawakupenda kukaa chini na kunyeshewa na mvua wakiomba msaada.

Posted by Bigie on 12:22 PM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.