POMBE YAMTOA MADEE...ANADAI IMEMPA HESHIMA KUBWA MTAANI


Msanii wa Kundi la Tip Top Connection, Madee au Rais wa Manzese ameeleza kuwa wimbo wake wa Nani Kamwaga Pombe Yangu umempa heshima kubwa.
  
Akiongea  na  mwandishi  wetu, Madee, ambaye jina lake halisi ni Hamad Ally Seneda alisema licha ya kupata shoo nyingi, lakini pia ni wimbo ambao unapigwa sana kwenye klabu mbalimbali na kila unapopigwa hakuna anayekaa kitini.
Alisema kuwa kufuatia kutoa wimbo huo ameshakusanya Shilingi 16 milioni.
Alisema pamoja na kupata fedha nyingi kupitia wimbo huo bado hajaamua azifanyie nini ila ameamua atulie kwanza akitafakari nini kinafuata.
“Wimbo bado upo juu na unafanya vizuri, hivyo ninachofanya kwa sasa ni kuendelea kukusanya fedha kutokana na shoo ambazo nitapata kutoka kwenye wimbo huo baada ya hapo ndio nitajua nifanyie nini,” alieleza.
Aidha, Madee alisema kuwa anafurahi kuona amefanya kitu ambacho kila mpenda burudani kinamfurahisha kwani sio wasanii wengi ambao wanaweza kufanya kitu kama hicho hasa kwa wale waliopo kwenye usanii kwa muda mrefu. Kalunde Jamal

Posted by Bigie on 1:16 PM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.