VURUGU NA MIGOGORO YASABABISHA MAJENGO MATATU YA SHULE YA SEKONDARI YA IFUNDA KUCHOMWA MOTO


Majengo matatu ya  Sekondari ya Ufundi Ifunda, mkoani Iringa yamechomwa moto  kwa siku tatu mfufulizo na kuteketea  kabisa, huku  chanzo  cha matukio hayo kikitajwa kuwa ni  hujuma kutokana na mgogoro uliopo shuleni hapo.
  
Shule hiyo ya mchepuo wa sayansi ambayo ilianzishwa mwaka 1950, imeingia katika migogoro baina ya uongozi wa shule hiyo na wafanyakazi na baadhi ya wanafunzi. 

Wanafunzi 10 walisimamishwa hivi karibuni 10 kutokana na utovu wa nidhamu,  hatima yao inasubiri kikao cha bodi ya shule  Aprili 17, mwaka huu.
 
Wakati wanafunzi hao wakiwa wamesimamishwa, walimu watatu wamepewa barua za uhamisho ikitajwa kama sehemu ya kuboresha ikama ya ualimu shuleni hapo.
 
Kaimu mkuu wa shule hiyo,  Twaha Mruma alimweleza  Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Gerald Guninita aliyefika shuleni hapo   jana kujionea kiwango cha uharibifu huo kuwa, matukio ya kuchomwa moto majengo hayo ni  hujuma. Alisema matukio hayo yalianza Mwezi Aprili 4, mwaka huu na yamefanywa kwa siku tatu mfulululizo

Posted by Bigie on 11:58 PM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.