WEMA SEPETU ATOA PICHA KUONESHA ALIVYOJERUHIWA.....ASISITIZA KUMSHITAKI MAMA YAKE MZAZI


Picha aliyoweka Wema Sepetu Instagram kuelezea ugomvi uliotokea, na kuandika: ” Da fight I got into today caused me da marks I hav on my baq… things I do for da people I love always cost me… nd u knw wat ama kip doin.”

Staa huyo wa Bongo Movie ambaye pia ni mmilikiwa kampuni ya Endless film, amemfikisha mama yake mzazi anayejulikana kama Miriam Sepetu kwenye Kituo cha Polisi Kijitonyama jijini Dar es salaam kwa madai ya kwenda nyumbani kwake na kufanya vurugu zilizosababisha kuharibika kwa samani nadani ya nyumba yake.

Tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia Jumatano iliyopita, nyumbani kwa Wema, Kijitonyama, jijini Dar.

Mbali na mama mtu, wengine waliofikishwa kituoni hapo ni dada mkubwa wa Wema aitwaye Nuru na kijana aliyefahamika kwa jina moja la Bestizo ambaye inasemekana ni mshirika mkubwa wa Diamond kwenye masuala ya mtandao wa msanii huyo.

Wema alikwenda polisi na kuandikisha maelezo ambayo yameingizwa kwenye jalada lenye kumbukumbu; KJN/RB/2755/2013 SHAMBULIO, KUHARIBU MALI.

Posted by Bigie on 10:33 AM. Filed under , . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.