AFANDE SELE AGOMA KULA BAADA YA SIMBA KUPAKATWA NA YANGA


King Selemani ama Afande Sele kutoka mji kasoro bahari Morogoro ni moja ya watu wanaoonekana kuwa ‘addicted’ na ushabiki wa soka kiasi cha kushindwa kuvumilia maumivu ya kufungwa kwa timu anayoishabikia, Simba kitendo kilichompelekea asuse kula toka Jumamosi.

Akizungumza na Suddy Brown katika segment maarufu ya U Heard kupitia XXL ya Clouds FM, mke wa rapper huyo mkongwe Mama Tunda, amethibitisha kuwa mumewe amegoma kula toka siku ya mechi. 
Mbaya zaidi kwa Afande ni kuwa Mama Tunda na binti yao Tunda ni mashabiki wa Yanga hivyo wao na Selemani Msindi ni mashabiki wa timu mbili pinzani, hatupati picha humo ndani panavyokuwa ikifungwa timu anayoshabikia baba wa familia!. Minuno ya hatari bila shaka. Pole Afande.

Posted by Bigie on 12:49 PM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.