SERIKALI YAPIGA MARUFUKU MIKUTANO YA DINI YENYE "VIRUSI" VYA UCHOCHEZI


Waziri wa MAmbo ya Ndani ya NChi, EMmanuel NChimbi, ameliagiza jeshi la polisi kuanzia IGP, RPC, OCD na OCS kuwachukulia hatua wale wote wanaoendesha mihadhara ya kidini yenye kuchochea vurugu na mifarakano katika jamii. ...


Nchimbi amesema kuwa kiongozi yeyote ambaye atabainika kutochukua hatua licha ya taarifa kuripotiwa kwake basi atakwenda na maji.. ...


Kauli  hiyo  ameitoa   jijini dar es salaam jana wakati akiongea na wawakilishi wa viongozi wa dini na vyombo jeshi la polisi mkoa wa dar es salaam

Waziri Nchimbi amewatahadhalisha vijana wanaoshinda kwenye mitandao na wanaotumia simu kutuma ujumbe wenye lengo la kuhamasisha chuki za kidini. Amesema kuwa kuanzia sasa serikali itachukua hatua
   stahiki

Chanzo: taarifa  ya  habari ya TBC1   ( saa  nne asubuhi)

Posted by Bigie on 12:56 AM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.