WASANII WATAKAOTUMBUIZA KATIKA SHOW YA UFUNGUZI WA BIG BROTHER WATAJWA

Show ya ufunguzi wa msimu mpya wa shindano la Big Brother Africa itafanyika Jumapili hii, May 26 nchini Afrika Kusini. 

Usiku huo utawaonesha washiriki wote 28 watakaoanza safari ya miezi mitatu ya kuzisaka dola laki tatu za msimu wa nane wa Big Brother Africa, The Chase.


Miongoni mwa wasanii watakaotumbuiza kwenye ufunguzi huo ni pamoja na STL wa Kenya, Don Jazzy, D’ Prince na Wande Coal kutoka Nigeria na kundi la Mafikizolo la Afrika Kusini.
Wande-Coal-Album
Pia mchekeshaji wa Kenya Daniel Ndambuki, maarufu kama Churchill atapanda kwenye stage kuwavunja mbavu watazamaji wa show hiyo katika nchi 50 barani Afrika. 

Show hiyo itaonekana live pia kupitia website ya Big Brother,.

Posted by Bigie on 6:33 AM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.