"MILIO YA SIMU YENYE MAUDHUI YA KIDINI IPIGWE MARUFUKU"...JAMES MBATIA

Mbunge wa kuteuliwa Mh. James Mbatia, (akichangia bajeti ya Wizara ya Mambo ya Ndani),ameitaka serikali kuchukua hatua kuhakikishi milio ya kupokelea simu yenye maudhui ya kidini pale unapompigia mtu simu isitishwe nara moja....
Mh.Mbatia ameyasema hayo leo bungeni wakati akichangia bajeti ya wizara ya mambo ya ndani.
Mh.Mbatia ametoa mfano kwamba hata sasa unaweza kumpigia simu afisa wa ngazi ya juu wa jeshi la polisi na utakuta simu yake inatoa mlio wenye maneno au ujumbe wa dini yake.


Mh.Mbatia alitoa mfano wa maneno kama "pepo toka" maneno ambayo mtu huyasikia pale unapompigia mtu simu  na  kudai  kuwa  yanachochea  vurugu  za  kidini  na  kuleta  mgawanyiko  miongoni  mwa  watanzania

Posted by Bigie on 3:16 AM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.