SAUTI YA SAIDA KAROLI AKITHIBITISHA KUWA NI MZIMA NA HAJAFA KAMA WATU WANAVYODAI....


Mwanamuziki mkongwe wa nyimbo za asili nchini Saida Karoli, amezikanusha tetesi zilizoanza kuenea tangu jana kuwa amefariki kwenye ajali ya boti katika ziwa Victoria.

Akiongea kwa simu  leo asubuhi , Saida ambaye baada ya kutumbuiza kwenye tuzo za Kili wiki iliyopita alielekea Makongorosi Chunya mkoani Mbeya, amesema yupo hai na ni mzima wa afya.

“Mungu wangu, mimi niko hai, ndugu yangu, naomba uwaeleze watanzania kwamba Saida ni mzima, hakuna chochote kilichotokea hata mimi mwenyewe nimeshangaa yaani watu wanapiga simu, ni suala la msiba lakini si kweli,” amesema Saida.



Credit: Bongo5

Posted by Bigie on 3:57 AM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.