TASWIRA KUTOKA MSIBANI KWA MAMA MZAZI WA JAFFARI ALLY (MUME WA KHADIJA KOPA)

 Mama Mzazi wa marehemu Jaffari Ally, Bi. Rehema Tuwa, akilia kwa uchungu nyumbani kwake Tandale jijini Dar.

 Simanzi na majonzi vilitawala msiabani hapo.
Akina mama waliofika kumpa pole Mama Mzazi wa Jaffari.

SIMANZI, vilio na majonzi vilitawala nyumbani kwa Mama Mzazi wa marehemu Jaffari Ally, Bi. Rehema Tuwa, Tandale jijini Dar. 

Marehemu Jaffari ambaye alikuwa ni mume wa Malkia wa Mipasho nchini, Khadija Kopa amefariki dunia usiku wa kuamkia jana  katika hospitali ya Jeshi ya Lugalo.

 Marehemu Jaffari alikuwa Diwani wa kata ya Magomeni wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani wakati mama yake mzazi ni Mwenyekiti wa UWT Tandale.


 Mungu ailaze roho ya marehemu Jaffari Ally mahali pema peponi. AMEN!

Posted by Bigie on 6:32 PM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.