TUZO ZA KILIMANJARO MUSIC AWARDS ZITARUSHWA LIVE MTANDAONI....


Usiku wa tuzo za Muziki Tanzania maarufu kama Kilimanjaro Tanzania Music Awards 2013 unatarajiwa kuonyeshwa live mtandaoni siku ya Jumamosi, Juni 8.



Tofauti na miaka mingine ambayo tukio la utoaji tuzo tu ndio lilikuwa likionyeshwa kupitia kwenye TV pekee, na kuwanyima fursa Watanzania waishio nje ya nchi kufuatilia moja kwa moja, mwaka huu watumiaji wa mtandao wa Internet wataweza kuangalia toka mwanzo tukio la Red Carpet litakaloanza saa moja jioni wakati wanamuziki na watu wengine mashuhuri wakiwasili ukumbini.



Pia tukio la utoaji tuzo litakaloanza rasmi saa tatu usiku litakuwa moja kwa moja mtandaoni hadi litakapofikia mwisho. 


Watumiaji wa simu za Android, Blackberry, iPhone na tablets wanaweza ku-download application ya *LIVESTREAM* itakayowawezesha kuangalia moja kwa moja kwenye simu zao wakati watumiaji wa computer watatazama kupitia http://new.livestream.com/KTMA2013/live na katika Blogs mbalimbali

 
Pia picha za matukio yatakayokuwa yakijiri ukumbi zitapatikana kupitia ukurasa wa Instagram wa Kilimanjaro Premium Lager ambao ni www.instagram.com/kili_lager   wakati ule wa Twitter www.twitter.com/kili_lager utakuwa ukitoa habari zinazoendelea na washindi wa tuzo na itapatikana pia katika ukurasa wa Facebook wa Kilimanjaro Premium Lager.

Posted by Bigie on 12:44 AM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.