MR. NICE APATA SHAVU JINGINE NCHINI KENYA BAADA YA KUTEMWA NA GRANDPA


Ikiwa ni zaidi ya mwezi mmoja toka staa wa Bongo Luca Mkenda aka Mr Nice apoteze nafasi ya kufanya kazi na label ya GrandPa ya Kenya kwa shutuma za uvivu, kushindwa kutoa ushirikiano na ukiukaji wa mkataba hatimaye mlango mwingine umefunguka kwa nyota huyo wa ‘Kikulacho’.


Mr Nice ambaye bado yuko Kenya anatarajia kujiunga na label nyingine nchini humo ‘Candy Records’ ambayo ina miezi michache toka ianzishwe. 


Kwa mujibu wa CEO wa label hiyo John Kariuki aliyekuwa akizungumza katika ufunguzi rasmi wa label hiyo jijini Nairobi, alisema wako katika hatua za mwisho kukamilisha mpango wa Mr Nice kusain mkataba nao kama ilivyoripotiwa na Niaje.


Label hiyo tayari imesha wasain wasanii kadhaa wa Afrika Mashariki akiwemo hit maker wa ‘Ulofa’ Top C wa Tanzania, pamoja na wengine kutoka Kenya.

Posted by Bigie on 11:43 PM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.