ODAMA AWAJIBU WANAOMTUHUMU KUZIFANYIA " PHOTOSHOP " PICHA ZAKE NA KUDANGANYA ALIKUWA ULAYA


Baada ya kuzagaa kwa habari zikimtumu mwanadada wa filamu Tanzania Jennifer Kyaka aka Odama kwamba huzifanyia makeke ya photoshop picha zake na kuwadanganya wananchi kuwa amezipigia Ulaya, ameongea na na  mwandishi wetu  kukanusha huku akionesha picha halisi zinazomuonesha akiwa mbele.
 

Baada ya tuhuma hizo kumkabili Odama, Mwandishi wetu alimtafuta mwanadada huyo wa filamu na ndipo alipokanusha tuhuma hizo na kusema hakufanya kitu kama hicho na kwamba waliosema hivyo wanania mbaya naye.


Ili kukata ‘ngebe’ za manisnitch hao Odama ametutumia  picha hizi za ushahidi kwamba alikuwa nje ya nchi kama alivyosema.


“Kuna watu wanakosa vya  kufanya ndio maana wanakaa na kuanza kuzusha vitu ambavyo hawana uhakika navyo so siwashangai kwakuwa binadamu tunatofautiana upeo,” Odama
 
 

Bongo5

Posted by Bigie on 8:12 AM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.