"NAWACHUKIA SANA WASANII WA BONGO MOVIE MAANA NI WEZI WA WAUME ZA WATU"...AMANDA

 
 MSANII wa filamu za Kibongo, Tamrina Poshi ‘Amanda’ amesema anawachukia sana wasanii wa kike wa Bongo Movie kutokana na tabia zao za kuchukuliana mabwana.


Amanda alisema wasanii wengi wa filamu wana tabia za kuibiana mabwana kitendo ambacho kinamkera na kusababisha kuwachukia kwani wanavyofanya siyo heshima na inawaharibia sifa kwa jamii pamoja na kuichafua tasnia yao kwa jumla.
 


 “Nawachukia na ndiyo maana sitaki kuwa na rafiki Bongo Movie kwa sababu wamekuwa na tabia mbaya sana mifano halisi ipo lakini siwezi kuitaja,” alisema.

Mbali na hivyo, Amanda alisema kuna wasanii wawili wa kike walikuwa marafiki sana hata kwenye mitandao walikuwa wakiitana mawifi lakini hivi sasa hawaivi, kisa  kunyang’anyana bwana

GPL

Posted by Bigie on 12:31 AM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.