Baba afikishwa mahakamani baada ya kumbaka mwanae

MKAZI wa Kijiji cha Njoro wilayani Kiteto mkoani Manyara, Mohamed Ally (42) amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi kwa tuhuma za kumbaka mtoto wake wa kufikia. 

Mwendesha Mashitaka wa Polisi, Paulo Kimaro alidai mahakamani kuwa tukio hilo lilitokea Septemba 9 mwaka huu nyumbani kwa mtuhumiwa huyo alipombaka mtoto huyo, mwanafunzi wa darasa la saba.
 

Alidai siku hiyo mke wake alitoka na aliporejea kutaka kuingia ndani alisukumwa nje na baada ya kulazimisha kuingia ndipo akagundua kuwa mumewe alikuwa anafanya mapenzi na mtoto wake huyo

Kimaro alidai kutokana na hali hiyo aliomba msaada ofisi ya kijiji cha Njoro na mtuhumiwa akakamatwa na kufikishwa polisi na baadaye mahakamani.

Mtuhumiwa alikana mashitaka na alirejeshwa rumande hadi Septemba 23 mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa tena.

Mke wa mtuhumiwa, Salima Hamisi aliiambia mpekuzi blog kuwa mwanafunzi huyo ni mtoto wa kulea na walimchukua akiwa na umri wa miaka miaka minne.

Kwa mujibu wa taarifa mwanafunzi huyo alifanya mtihani wa taifa wa darasa la saba kwa siku ya pili jana.

Posted by Bigie on 11:38 PM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.