Gari la Operation kimbunga lapinduka na kuua askari watatu...Chanzo cha ajali ni Bibi kizee

 
Askari Polisi watatu wa Operesheni Kimbunga wamefariki dunia jioni ya juzi  mjini Kahama baada ya kupata ajali ya gari walilokuwa wakisafiria kutoka Muleba mkoani Kagera kuelekea makambako mkoani Njombe. 

Ajali hiyo imetokea katika eneo la Sungamile Kata ya Kagongwa wilayani Kahama wakati dereva wa gari hilo PF3270 PC Yusuph, akijaribu kumkwepa Bibi Kizee mmoja huku gari likiwa kwenye mwendo kasi na hivyo kumshinda na kupinduka.

Majeruhi wanane wamelazwa katika Hospitali ya wilaya ya Kahama wakiwemo askari polisi sita na Maafisa Uhamiaji wawili, huku magari yanayosafirisha askari kurudi vituoni kwao yakizuiliwa kuendelea na safari na kulala Kahama.


Posted by Bigie on 2:01 AM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.