Hawa ndo watuhumia wa EPA waliohukumiwa kwenda jela....Wawili kati yao ni mume na mke

Washtakiwa watatu kati ya watano waliokuwa wakikabiliwa na kesi ya wizi wa fedha kwenye Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) wamehukumiwa kifungo jela baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwatia hatiani ambapo kati yao ni mke na mume. 



Kushoto ni Bahati John amehukumiwa kifungo cha miaka 7 na katikati ni Manase Mwakale amehukumiwa miaka 5 na mkewe Eddah Mwakale amehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja. 

Manase Mwakale akiongea na wakili wake baada ya kuhukumiwa kifiungo cha miaka mitano jela.

Eddah Mwakale akiongea na wakili wake. Kulia ni Mume wake, Manase Mwakale ambaye amehukumiwa kifungo cha miaka 5 jela.

Washtakiwa wakitoka mahakamani baada ya kusomewa hukumu yao.

Posted by Bigie on 4:53 PM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.