Irene Paul ajiona mwenye bahati baada ya kupata nafasi ya KUTOMASWA na Van Vicker ambaye ni staa wa Nigeria

 
Msanii wa sinema za Kibongo, Irene Paul amesema ameridhishwa na uwezo wa mkali wa sinema za Kinigeria, Joseph Van Vicker akidai ni jasiri na mjuzi sana katika scene  za mapenzi.

Akizungumza na mwandishi wetu, Irene alisema kuwa pamoja na kuigiza naye kwa mara ya kwanza ‘scene ya on bed’ lakini Vicker alionesha uzoefu wa hali ya juu utadhani wanafahamiana kitambo, jambo lililomshangaza na kujikuta akiingiwa na woga.
  “Jamaa utadhani tunafahamiana, alinikabili kitandani kwa kiwango kikubwa sana, nilipata hofu kubwa mno. Van anajua kuigiza jamani, kwangu hii ni bahati ambayo namshukuru Mungu kuipata, wengi waliililia,” alisema Paul.
 

Van aliibuka Bongo na kuondoka wiki iliyopita kwa ajili ya kushuti sinema moja na wasanii wa nyumbani ambayo bado haijapatiwa jina.

Posted by Bigie on 1:16 AM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.