Jiji la Dar lina MENGI...Mama anaswa AKIMNYONYESHA MBUZI.....Aliposhiba alichukua mbeleko na kumtia mgongoni.

 
Na Rashid Mkwida — Katika hali isiyozoeleka, mwanadada huyu alikutwa na kamera ya Mkwidna blog katika mitaa ya Jijini Dar es salaam akihaha na mwanambuzi mgongoni huku mwanambuzi huyo akilia mee meee!!
 Mwanadada huyo alilazimika kumbembeleza kwa  kujaribu  kumnyonyesha mwanambuzi huyo aliyekuwa akilia kwa sauti kiasi cha kuwashangaza wapita njia..

 Kuna wakati mwanambuzi huyo alitaka kuchoropoka katika mbeleko ya mwanadada huyo lakini mwanadada huyo alijitahidi kuifunga vyema mbeleko yake ili mwanambuzi huyo akae vyema, haikufahamika mara moja mwanadada huyo alikuwa akimpeleka wapi mwanambuzi huyo.


Posted by Bigie on 5:28 AM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.