Mzungu wa African Barrick Gold atiwa mbaroni kwa kumtelekeza mtoto aliyezaa na binti wa KITANZANIA
habari za kitaifa 4:08 AM
Andre akiwa na mtoto wake nje ya mahakama
BULHYAHULU Mzungu akitoka kusikiliza shauri lake chumba cha mahakama ambapo shauri hilo liliahirishwa mpaka tarehe 4.10.2013 ambapo alidhaminiwa na wadhamini wawili .
Raia wa nchini Canada ambaye ni mfanyakazi wa kampuni ya African Barrick Gold Bulyanhulu aliyefahamika kwa jina la Andrew Lapierre (50) amefikishwa mahakama ya mwanzo Lunguya wilayani kahama mkoani shinyanga kwa kosa la kutelekeza mtoto kinyume cha kifungu namba 166 cha sura ya 16 aliyezaa na Bi Elizabeth John.
Akisoma makosa ya mtuhumiwa, hakimu wa mahakama ya mwanzo Lunguya Derick Masaga ameiambia mahakama kuwa Andre Lapierre mwaka jana alimpa hujauzito Elizabeth John (21) mkazi wa Kakola ambaye alizaa mtoto wa kike aliyefahamika kwa jina la Mariam Andre, na kumtelekeza muda wote bila huduma.
Mtuhumiwa alikana kumtelekeza mtoto huyo na kuiomba mahakama hiyo iagize wakapimwe vipimo vya vinasaba (DNA) ili kubaini ukweli na vipimo vimethibitisha hilo.