Tazama jinsi Al shabaab walivyoiteka Kenya (West gate) pamoja na majina yao...Video fupi muhimu


Jumamosi takriban saa tano unusu asubuhi, genge la kigaidi linaloshukiwa kuwa la Al Shabaab lilipata kungia katika eneo la kibiashara la Westgate wakiwa kwenye magari ya kibinafsi.

Kundi hilo la takriban watu 10-15 liliweza kuingia kupitia lango kuu la jumba hilo huku lingine likiingia kutoka eneo la kuegeshea magari lililoko paani.
 

Katika lango kuu walianza kwa kumuua mkurugenzi wa kampuni ya usalama inayolinda eneo hilo kabla ya kuelekea paani ambapo ulikuwa na hafla iliyoandaliwa na idhaa ya East FM.
 

Wale walioingilia lango kuu wakafululiza hadi duka la Nakumatt lililoko katika jengo hilo na ni hapa ambapo mauaji ya Wakenya wasiokuwa na hatia yoyote yalipoendelezwa zaidi.

Milio ya risasi ikasheheni angani.
Huku haya yakijiri tayari maafisa wa polisi walikuwa wamepata habari hizo na vikosi mbali mbali vikakita kambi na kulizingira eneo hilo, magharibi, mashariki, kusini na hadi angani.


Shughuli ya uokozi ikaanza ili kufanikiwa kuwashikilia mateka kwa siku tatu mtawalia huku vikosi vya usalama vinajua ina maana kuwa magaidi hawa walikuwa wamejihami vilivyo.


Na je ni akina nani hawa ? 
Duru za kuaminika zinaarifu kuwa, washukiwa hawa ni watu wa tabaka na mataifa mbali mbali wakiwemo wafuatao wanaodaiwa kushiriki kwenye shambulizi hilo:
1. Sayd Nuh - 25 - Kismayu
2. Ismael Galed - 23 - Finland
3. Mustafa Noordiin - 24 -  Marekani
4. Abdifatah Osman- 24 - Marekani
5. Kassim Musa - 22 - Garissa
6. Mohammed Badr - 24 - Syria

Aidha waziri wa masuala ya ndani na usalama Joseph Ole Lenku amefutilia mbali madai kuwa kiongozi wa kundi hilo ni mwanamke akishikilia kwamba ni wanaume waliovalia mavazi ya kike.


Kufikia sasa  vikosi vya kenya vya usalama vimechukua usukani wa orofa zote za jengo hilo, na kulingana na Lenku ni kuwa magaidi wangali wamejificha, japo wawili tayari wameuawa.

Posted by Bigie on 1:09 PM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.