Wanawake Elfu 8 nchini Nigeria waandamana kuishinikiza Serikali iwasaidie WAOLEWE....( Sipati picha ingekuwa Tanzania )

  Nigeria ina upungufu wa wanaume wa kuoa kiasi kwamba wanawake wanaotamani kupata wenza na kutengeneza familia wameamua kuchukua hatua.  

Zaidi ya wanawake elfu 8 walio single jana wameandamana kutokana na upungufu wa wanaume wa kuwaoa.  

Lengo la maandamano yao ni kuishinikiza serikali kuwasaidia waolewe, kivipi? (Ndio swali hata mimi nimejiuliza!)  

Wanawake waliojikusanya na kuandamana ni mkusanyiko wa 5380 waliopewa talaka, 2200 ni wajane 1200 yatima, na 80 wengine.  

Wanawake hao wamedai kuwa hawana uwezo hata wa kununua chakula cha siku kwa sababu hawana wanaume wa kuwasaidia ndio maana wanahitaji wanaume wa kuwaoa na kuwasaidia mahitaji yao.  

 SOURCE: NAIJA GISTS

Posted by Bigie on 6:07 PM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.