Natafuta Dancers Wa Kike Kwa Muda Mrefu Ila Bado Kupata Wenye Viwango Vya Kimataifa: Diamond Platnumz.
burudani 9:25 PM
Licha ya kuonekana na madansa wa kike katika jukwaa la Fiesta 2014 Mwanza, Diamond anasema hajabahatika kumpata dansa wa kike mwenye vigezo anavyovitaka.
“Sina madansa wa kike pale wawili ni wa Vanessa naweza sema wote si 
wangu, zamani nilikuwa na madansa wa kike, lakini kwa sasa Tanzania tuna
 upungufu kwenye muziki wa Bongo Fleva na muziki wa bendi kuna madansa 
ambao wamebobea kucheza muziki wa dansi pekee. Nilitamani kuwa na 
madansa wa kike zamani lakini ilishindikana maana kuwapata ni ngumu 
sana,” anasema na kuongeza:
“Mpaka sasa bado natafuta madansa wa kike sijawapata, nahitaji dansa wa 
kike ambaye anajua, awe anajiamini afuatilie madansa wa nje wanachezaje,
 awe na unyamwezi kidogo ni ngumu sana, awe mbunifu afuatilie muziki wa 
nje na vitu kama hivyo. Kwa hiyo nikatamani nifanyaje nikaamua kuazima 
madansa wa watu nifanye nao shoo,” anasema.
Akiwazungumzia madansa wake wa kiume ambao ni sita, Diamond anasema ni 
madansa wanaolipwa pesa ndefu ukilinganisha na madansa wote Afrika 
Mashariki.
"Siwezi kusema nawalipa kiasi gani itakuwa kama nawavua nguo, lakini 
hakuna madansa wanaolipwa vizuri kama wangu Afrika Mashariki, ikiwa bei 
inaongezeka na mimi nawaongeza katika malipo yao. Wako sita kwa kweli 
nimetoka nao mbali tangu ‘Kamwambie’ mwaka 2009, nimekua nao kifikra, 
kiumri na kiakili na kuona kwamba hawa ni mzigo wangu mimi na wanafanya 
kazi pamoja na mimi, wale ni mafanikio yangu wana msaada mkubwa sana 
pengine nisingekuwa hapa bila wao,” anasema.
Hata hivyo, anaweka wazi kwamba linapofika suala la shoo za nje, huwa 
inategemea ni wapi kwani shoo zingine hairuhusiwi kwenda na madansa wote
 hivyo huwa anawabadilisha kwa zamu.
Katika mahojiano hayo maalum na Mwananchi, superstar huyo alisema kuwa kwasasa muziki wa Bongofleva unakubalika nje ya nchi tofauti na zamani.






