Video: Magaidi wa ISIS Wamchinja na kumkata Kichwa Mateka Mwingine Raia wa Uingereza


Taarifa zilizopatikana hivi punde zinaeleza kwamba kikundi cha kigaidi cha Dola ya Kiislamu (ISIS) kimemchinja kwa kumkata kichwa, David Haines, Mwingereza mfanyakazi wa shirika la misaada, kwa mujibu wa video iliyosambazwa na kikundi hicho.
 
Video ya mauaji hayo ya kinyama inaanza kwa kuonyesha hotuba ya Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron kuhusu Iraki, ikifuatiwa na ujumbe kwa washirika wa Marekani dhidi ya kikundi hicho, na inahitimishwa kwa tukio la kuogofya la kukatwa kichwa kwa Davidi ambaye ni Mskochi.
 
Tukio hilo limetokea na kurekodiwa katikati ya jangwa. Baada ya hotuba ya Cameron, mtu aliyejifunga kitambaa kuficha uso huku ameshikilia kisu anaonekana amesimama mbele ya David ambaye amepiga magoti, na kuamriwa kusoma 'hotuba ya mwisho.'
 
Katika hotuba hiyo fupi, Mwingereza huyo anasema, namnukuu, "Ninapenda kubainisha kuwa ninakulaumu Davdi Cameron kwa kuuawa kwangu.Umeingia kwa hiari katika ushirika na Marekani dhidi ya Dola ya Kiislam, kama alivyofanya mtangulizi wako Tony Blair."
 
Baada ya kusoma taarifa hiyo, Davidi anakatwa kichwa kisha Mwingereza mwingine, Alan Henning anaonyeshwa akitishiwa maisha. 
 
Mtu aliyefanya uchinjaji huo anaonekana kuwa ni yuleyule aliyewachinja watu wengine wawili kabla ya tukio hili. 
 
Kadhalika, anasikika akitoa onyo, namnukuu, "Iwapo wewe Cameron utaendelea kupambana na Dola ya Kiislam, basi wewe, kama bwana wako Obama, mikono yenu itakuwa na damu ya watu walio mateka wetu."

Tazama  Video  hapo  chini( Video Inatisha) 
 

Posted by Bigie on 10:42 PM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.