BAKWATA Yasisitiza kuwa Maamuzi ya Rais Kikwete kuhusu Sakata la Escrow Yaheshimiwe


BARAZA Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) limewataka Watanzania kuheshimu uamuzi wa Rais Jakaya Kikwete na mamlaka zinazohusika kuhusu suala la akaunti ya Tegeta Escrow.
 
Kauli hiyo imetolewa na Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Musa Salum ambapo alisema, ni muhimu kwa Watanzania kumuamini Rais Kikwete na kuziachia mamlaka husika kufanya kazi zilizoagizwa.
 
Akigusia hotuba hiyo, alisema ni hotuba nzuri ambayo imekusanya historia nzima ya fedha za Kampuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) na kufafanua kama ni za umma au si za umma, pia imeonesha ukomavu.
 
Alisema kama Bakwata wanapongeza hotuba ya Rais Kikwete kwani ameonesha ni kiongozi anayetumia hekima na weledi katika uongozi na kutatua matatizo mbalimbali, licha ya kuwepo kwa mashinikizo kutoka kwa watu mbalimbali.
 
“Kiongozi yeyote hapaswi kukurupuka katika kutoa maamuzi na hilo ndilo alilolionesha Rais Kikwete katika hotuba yake.

“Hakuna sababu ya watu kuandaa maandamano kwani aliyoyasema Rais Kikwete yameeleweka na alieleza kwa upana zaidi, hivyo watu wasitake kumsambazia ubaya hata kwa mazuri anayoyafanya tayari; mamlaka zinazohusika zimepewa majukumu na wengine wamewajibishwa,” alisema Salum.
 
Alisema pia baraza hilo litaendelea kupinga mambo ambayo yanaonekana kutaka kuchangia kupoteza amani ya nchi, kwa lengo la kuidumisha na kuienzi siku zote.

Posted by Bigie on 6:15 PM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.