AISHA MADINDA ACHOSHWA NA TABIA YA KUPORWA WACHUMBA
JAMII 1:16 AM
MWANAMUZIKI wa Bendi ya Extra Bongo ‘Wazee wa Kizigo,’ Aisha Mohammed Mbegu ‘Aisha Madinda’ amefunguka kuwa kati ya vitu ambavyo vimekuwa vikimkosesha raha katika maisha yake ni kuporwa wachumba.
Akizungumza na mpekuzi wetu, Aisha alisema kuwa hali hiyo imekuwa ikimkumba kutokana na tabia yake ya kupenda kuwatambulisha wapenzi wake kwa mashosti zake.
Alisema: “Unajua kuna baadhi ya wanenguaji wenzangu ni micharuko, mchumba wangu wa kwanza nilipomtambulisha kwao wakanipora, wa pili naye hivyo hivyo, iliniuma sana lakini nimejifunza kitu.
“Sasa hivi nina mchumba wangu ambaye ameshafanya taratibu za kutaka kuishi na mimi kama mke na mume, huyu sitamtaja kwa sasa maana naye wanaweza kuniibia.”