ASKOFU PENGO AONYA JUU YA MCHAKATO WA KATIBA MPYA
JAMII 12:19 AM
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Katholiki Dar es Salaam, Mwadhama POLYCARP KARDINAL PENGO amesema mchakato wa Katiba Mpya usipokamilika ndani ya miaka Mitatu, Uchaguzi Mkuu ujao utaghubikwa na uvunjifu wa amani, fujo na utata wa Katiba ipi inastahili kutumika.
Askofu PENGO ametoa kauli hiyo jana jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari ikiwa ni utaratibu wake wa kutoa Neno kila ifikapo kipindi cha Majilio ya Adventi kwa Wakristo ya kuelekea Sikukuu ya Krismas na Mwaka Mpya.
Amesema viongozi wa Serikali wanatakiwa kuwa makini na suala la mchakato wa Katiba Mpya kwani Taifa huenda likaingia kwenye machafuko ambayo awali taratibu sahihi zingefuatwa hali hiyo isingejitokeza.
Mbali ya suala hilo Askofu PENGO ameipongeza Serikali kwa kukataa kukubali shinikizo la Uingereza la kukubali kuhalalisha Ndoa za Jinsia moja kama ilivyokuwa ikishinikizwa kwa kigezo kuwa Taifa litakalokataa Ndoa za aina hiyo hazitapata misaada kutoka Uingereza.
Katika mkutano huo amesema Ndoa za Jinsia moja ni Tusi kuwa Mungu aliyeumba watu wa jinsia mbili tofauti hana uelewa hivyo wao wanaufahamu mkubwa zaidi ya Mungu.