"SINA MPANGO WA KUOLEWA"....AUNT EZEKIEL
JAMII 10:12 PM
KATIKA hali ya kushangaza msanii anayefanya vizuri katika tasnia ya filamu Bongo, Aunt Ezekiel amefunguka kuwa yeye si mwanamke wa kuolewa na katika maisha yake hana ndoto za kuja kuwa mke wa mtu.
Akiongea na Mpekuzi wetu hivi karibuni, Aunt alisema kuwa amefikia hatua ya kusema hivyo kwa kuwa anahisi kutopenda kuolewa.
Alisema, hali ya kuchukia maisha ya ndoa alikuwa nayo tangu alipokuwa mdogo na mpaka sasa anaamini suala la kuvishwa pete ya uchumba na hatimaye kuolewa halipo.
“Ninachoongea namaanisha, ndoa ni kitu ambacho hakipo kwenye akili yangu tangu nilipozaliwa, sijatendwa na mwanaume yeyote ila imetokea tu hivyo,” alisema Aunt.