ATHARI ZA MAFURIKO JIJINI DAR ES SALAAM:. 13 WAPOTEZA MAISHA -PICHA ZA TUKIO ZIMA
JAMII 10:14 PM
Wakaazi wa Dar es salaam wakitembea baada ya barabara ya Morogoro road sehemu za Jangwani kufungwa kwa muda kutokana na mafuriko yaliyoikumba jiji hilo kwa siku mbili mfululizo na hadi sasa imefahamika kuwa watu 13 wamepoteza maisha yao.
Boti kutoka feri likitelemshwa kusaidia zoezi la uokoaji
Askari wakiwa tayari kulinda usalama wa mali na watu
Mto Msimbazi ukifurika kuingia bahari ya Hindi
Daraja la Jangwani halipitiki
Askari wa JWTZ katika kuokoa wananchi
Boti za Fibre toka JWTZ zawasili kusaidia uokoaji
Gari la Serikali namba STK 3316 likiwa limetumbukia kwenye daraja lililobomoka kutokana na mvua iliyonyesha eneo la Makondeni kwa Mahita, Mbezi, Dar es Salaam. Dereva na abiria waliokuwemo walinusurika kwenye ajali hiyo.
Gari la Zimamoto mali ya Uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam likiwa limetumbukia kwenye daraja lililoharabiwa na mvua