AUNT APORA MUME WA MTU....


STAA wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel  amekwaa skendo ya kupora mume wa Mnenguaji wa Bendi ya African Stars International ‘Twanga Pepeta’, Fasha Joshua

Habari za moto kutoka kwa chanzo chetu, zinasema kuwa, licha ya kudaiwa kupora mwanaume huyo mwenye asili ya Kiarabu na kusababisha mfarakano mkubwa, pia Fasha amenyang’anywa gari aina ya Toyota Cresta namba T 895 BHG na kupewa Aunt.

“Ujue mume wa Fasha,  anaishi Dubai, alipokuja Bongo hivi karibuni inadaiwa alikutana na Aunt na kutoka naye. Huyu Aunt sasa amekuwa zoazoa. Awali walianzia kuchati kwenye Facebook baadaye wakakutana live.
“Alipokuja Dar, Aunt akamganda hadi ikafikia hatua jamaa akamuona Fasha si mali kitu, akamnyang’anya gari alilomnunulia na kumpa Aunt ambapo sasa anatanua nalo mitaani,” chanzo kilisema


Kikaendelea: “Siku chache baada ya jamaa huyo kuondoka Bongo, Aunt naye alisafiri kwenda Dubai anapofanyia kazi jamaa na huko ndipo walipomaliza kila kitu. Aunt alipewa kadi ya gari maana alipolinunua, kadi alibaki nayo, gari akampa Fasha.”


Chanzo kikazidi kusema: “Hapa ninapoongea na wewe, ukikutana na Aunt yuko na hilo gari, hasikii cha mtu, ukimuuliza kwa nini amemchukua bwana wa mwenzake, anajibu hajampora, kama ni gari alikabidhiwa na ndugu wa mwanaume hivyo yeye hahusiki na chochote.”


Kwa upande wake, mnenguaji huyo alisema anaamini Aunt amempora mwanaume wake, ndiyo maana alinyang’anywa gari na kupewa yeye.

Akasema, mbaya zaidi hata kwenye nyumba aliyokuwa akiishi (kwa wakwe zake), Mwananyamala- Komakoma aliondoka na kuhamia kwa dada yake, Kinondoni- Mkwajuni, Dar.


Mpekuzi  wetu alimtafuta Aunt na alikuwa na haya ya kusema:  “Hayo yote yanayosemwa ni uzushi mtupu, sijapora mume wa mtu na wala sina mpango huo.

Hilo gari nimeuziwa na huyo bwana wa Fasha na ndiyo maana niko nalo, sijapewa bure. Hakuna ukweli mwingine utakaoupata zaidi ya maneno yangu, labda umtafute huyo Fasha naamini atakuwa anafahamu wazi kuwa hilo gari nimeuziwa na hakuna mambo  nyuma ya pazia.

Iweje  nihongwe gari la Fasha wakati nafahamu alikuwa akilitumia? Huo ni uzushi tu, hauna ukweli hata kidogo.
"
Mwaka 2008 Aunt aliwahi kutoka na pedeshee maarufu Jack Pemba ambaye ilidaiwa ana mke Mzungu nchini Uingereza.

Mwaka 2009, Aunt huyu huyu akawa na uhusiano na bosi wa Kampuni ya Hartmann Production, Hartmann Mbilinyi ambaye pia ana mke anayeishi Uingereza.

Mwaka 2010, alifumaniwa na mwanamke anayeitwa Sarah Mwakapala ‘Bukabi’ akiwa kitandani na mchumba wake, Mwilu Mwilola ‘Silva’. Uchumba huo ulivunjika siku hiyo hiyo.

Posted by Bigie on 10:20 PM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.