BABY JOSEPH MADAHA NA MPENZI WAKE WAVAMIWA NA VIBAKA........VITU KIBAO VYAIBIWA


MSANII wa muziki wa kizazi kipya ambaye pia ni msanii wa filamu za Kibongo, Baby Joseph Madaha (pichani) na mpenzi wake ambaye jina halikufahamika mara moja, juzikati walivamiwa na vibaka kisha kuibiwa.

Rafiki wa karibu wa Baby alitutonya  kuwa, wawili hao walifanyiziwa nyumbani kwa msanii huyo Kinondoni jijini Dar muda mfupi baada ya kurudi kutoka kujirusha.

“Siku hiyo Baby akiwa na mtu wake walienda viwanja, waliporudi walikuwa bwii, wakaingia ndani kisha kuuchapa usingizi.
 
“Wakiwa wamelala vibaka walikata vyavu za dirisha wakawakomba vitu mbalimbali ikiwemo suruali ya jamaa yake iliyokuwa na fedha,” alisema reporter huyo.

Baada ya kuzipata taarifa hizi, mpekuzi wetu alimtafuta Baby ili azungumzie tukio hilo na alipopatikana alisema:
“Ni kweli tulipatwa na matatizo, hata sielewi ilikuwaje vibaka wakakata nyavu bila sisi kusikia, inawezekana walitupulizia dawa ya usingizi.”

Posted by Bigie on 10:03 PM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.