BASATA YAWAASA WASANII KUFANYA UTAFITI ILI KUBORESHA KAZI ZAO

Mkurugenzi wa Utafiti, Mafunzo na Habari wa BASATA, Godfrey Lebejo (Katikati) akizungumza na Wadau wa Jukwaa la Sanaa wiki hii kuhusu umuhimu wa Utafiti kwenye sekta ya Sanaa. Kulia ni Mratibu wa Jukwaa la Sanaa, Aristide Kwizela na Kaluona Desdery .
Mdau wa Jukwaa la Sanaa ambaye pia ni Mjumbe wa Shirikisho la Muziki, Francis Kaswahili akifafanua masuala mbalimbali kuhusu Utafiti kwenye Sekta ya Sanaa.
Wadau wa Sanaa wakifuatilia kwa makini Programu ya Jukwaa la Sanaa.


Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limeeleza kuwa, kuna kila sababu ya Wasanii kufanya utafiti wa kina kabla ya kuandaa kazi zao ili zikubalike kwa walaji na si kujifurahisha wao wenyewe.

Wito huo umetolewa wiki hii na Mkurugenzi wa Idara ya Utafiti, Mafunzo na Habari BASATA, Godfrey Lebejo wakati akizungumza na Wadau wa Sanaa katika ukumbi wa BASATA uliopo Ilala Bungoni kwenye program ya Jukwaa la Sanaa.

Lebejo alisema kuwa, utafiti ni muhimu pale msanii anapotafuta wazo la kuandaa kazi ili kujua itakubalika kiasi gani kwa jamii na ni ujumbe wa namna gani unakusudiwa.

“Msanii lazima afanye utafiti ili ajue mlaji wa kazi yake anataka nini. Hauwezi kutengeneza kazi ili kujifurahisha mwenyewe mwisho wa siku mlaji ni jamii inayokuzunguka” alisema Lebejo.

Aliongeza kuwa, madhara ya wasanii kutofanya utafiti husababisha kazi zao zisikubalike kwa jamii, zikose masoko, zidumu kwa muda mfupi lakini pia kuipotosha jamii kwa ujumla wake.

Aidha, aliongeza kuwa, vilio vya wasanii juu ya ukosefu wa masoko ya kazi zao, kujirudiarudia kwa kazi hizo na matatizo ya kunakili havitakwisha ikiwa wasanii hawatokuwa tayari kutumia muda wao katika kufanya utafiti.

Alisisitiza kuwa, utafiti ni moja ya mbinu za kutafuta maarifa mapya na suluhisho juu ya matatizo au changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii hususani wasanii na sekta ya Sanaa kwa ujumla.

Posted by Bigie on 1:32 AM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.