TATHMINI YA MAFURIKO DAR: IDADI YA WALIOKUFA YAFIKA 30 HUKU MAELFU WAKIKOSA MAKAZI
JAMII 5:50 AM
WALIOKUFA WAFIKIA 30,MAELFU WAKOSA MAKAZI
RAIS Jakaya Kikwete ametoa tamko kwa wakazi wanaoishi mabondeni, kwa kuwataka wahamie kwenye maeneo mapya watakayopangiwa ili kuepuka madhara zaidi.Wakati Rais akitoa tamko hilo, takwimu zilizokusanywa na gazeti la Mwananchi kutoka mamlaka mbalimbali tangu kuanza kwa mvua hizo mnamo Desemba 20, zinaonyesha waliokufa ni 30 lakini, Rais aliambiwa kuwa waliokufa ni watu 20.
Akizungumza jana katika shule ya msingi ya Mchikichini, Jijini Dar es Salaam alipokwenda kuwapa pole waathirika wa mafuriko yaliyotokana na mvua zilizonyesha kwa siku tatu, Rais Kikwete aliwataka watu kuhama mabondeni.
Shule ya Mchikichini ni miongoni mwa vituo vilivyotengwa kwa ajili ya kuwahifadhi waathirika wa mafuriko hayo.
Rais alisema: “Wakati Watanzania tunaomba usiku na mchana mvua iweze kunyesha ili mazao yaweze kustawi, wapo wenzetu ambao wanaomba jua liwake mwaka mzima.”
Alisema wanaombea jua liwake mwaka mzima, ili mvua isinyeshe kwa sababu wamejenga nyumba zao mabondeni ambako hawaruhusiwi.“Acheni kuishi kwa mashaka, ukiona wingu jeusi unaanza hofu, kila siku adui yako wewe ni mvua, tafadhali hamieni kwenye maeneo salama yatakayotengwa,”alisema Kikwete.
Mkuu huyo wa nchi aliongeza kwamba, katika maeneo mengine mafuriko yametokea kwa sababu watu wamejenga kwenye maeneo ya wazi na maeneo ya barabara.
“Maeneo hayo yakijengwa maji yanatafuta sehemu ya kupita, yakishindwa yanabomoa nyumba na miundombinu mingine,” alisema Kikwete.Alisema yote hayo yanafanyika huku viongozi wakiwemo watendaji wa mitaa na kata, wakiwa wanaangalia.
“Watu wanajenga na kuziba barabara, wengine wanajenga kwenye viwanja vya wazi kuna madiwani, watendaji wa kata na watendaji wa serikali za mitaa lakini hawachukui hatua zozote,” alisema Kikwete.
Rais Kikwete alisema hata kwenye maeneo hayo yanapotokea maafa, kazi ya uokoaji inakuwa ngumu kwa sababu maeneo yote yamejengwa nyumba.Alisema serikali itahakikisha waathirika wa mafuriko hayo wanapata huduma zote za kibinadamu zinazohitajika wakiwa katika vituo vua huduma.
Kabla ya kuzungumza na waathirika hao, Rais Kikwete alikagua maeneo ya jiji la Dar es Salaam yaliyokumbwa na mafuriko hayo kwa kutumia Helkopta.
RC Sadik
Kwa upande wake mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadik alimweleza Rais Kikwete kwamba ekari 2,000 za ardhi, zimetengwa katika wilaya ya Kinondoni kwa ajili waathirika wa mafuriko hayo.Alisema katika eneo hilo vitapatikana viwanja 2,800, ambavyo vitagawiwa kwa watu hao waliopatwa na maafa.
“Mheshimiwa Rais wapo baadhi ya watu wanaoishi mabondeni waliowahi kupewa viwanja ili wahame lakini, hawakufanya hivyo na viwanja walivyopewa waliviuza,” alisema Sadik.Alisema katika bonde la Msimbazi kila mwaka yamekuwa yakitokea maafa, ingawa hayakuwahi kutokea maafa makubwa kama ya sasa.
“Hatuwezi kuwa watu wa kusubiri maafa kila mwaka, ni lazima hatua sasa zichukuliwe ili wakazi wa mabondeni waweze kuhamia katika maeneo salama,” alisema Sadik.
Alisema kwa kuwa shule za msingi zitafunguliwa katika kipindi cha wiki mbili zijazo, waathirika hao watahamishiwa kwenye eneo maalum litakalojengwa kwa mahema.Sadik akizungumzia misaada ya kibinadamu ambayo imeanza kutolewa, alisema wameanza kugawa vyakula na maji.
Alisema mablanketi 1,600 yameanza kutolewa na magodolo yataanza kugawiwa katika maeneo mbalimbali hivi karibuni huku huduma za afya zikiwekwa katika kila kambi.Kuhusu miundombinu iliyoharibika, Sadik alisema wahandisi wa mkoa wameanza kufanya tathimini kufahamu uharibufu na hatua kuchukua.
“ Kuna madaraja kadhaa yamebomoka na barabara kuharibika, wahandisi wetu wanafanya tathimini ili tuweze kuchukua hatua za ujenzi,” alisema Sadik.
Waliokufa wafikia 30
Wakati Rais akielezwa waliokufa ni 20 takwimu ambazo Mwananchi imezikusanya kutoka mamlaka tofauti zinaonyesha kuwa mvua hizo, zimesababisha vifo vya watu 30 na majeruhi 50.Takwimu hizo zilipatikana katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Hospitali ya Amana, Hospitali ya Mwananyamala na Hospitali ya Temeke.Hata hivyo, Sadik alimweleza Rais Kikwete kuwa waliokufa katika mafuriko hayo ni watu 20 na walioathirika ni 4,909.Hata hivyo, Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela alisema jana kuwa tangu mvua zilipoanza kunyesha, mkoa wake wa kipolisi wa Kinondoni, kuliripotiwa vifo 13, vikiwamo vitatu vya watu wa familia moja ya Abeid Mntangi, mkazi wa Kimara.
Alisema familia hiyo ilikumbwa na maafa hayo baada ya ukuta wa nyumba yao kuwaangukia, kwa kusukumwa na maji ya mvua.Kenyela alisema katika eneo la Kimara Baruti, ulikutwa mwili wa mtu mmoja mwanaume mwenye umri wa kati ya miaka 55 na 60, ukiwa umekwama kwenye mizizi.
"Maiti hiyo ilikutwa haina nguo na haijatambuliwa vilevile, eneo la Kawe mtu mmoja mwenye asili ya Kimasai miaka kati ya 40 hadi 45 mwili wake umekutwa mto Kawe nao pia uko Mwananyamala," alisema.
Alisema pia eneo la Tabata Ami, mwili mwingine wa mwanaume mwenye umri kati ya 35 hadi 40 aliyekuwa amevaa fulana nyeupe na jinzi uliokotwa.
Katika eneo la Kigogo kwa Dua Said, Kamanda Kenyela alisema uliokotwa mwili wa mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka 12 ukiwa pembeni ya mto Msimbazi.Kamanda Kenyela alisema mwili wa Khalid Ali (22) ambaye ni mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Mgulani, ulikutwa ukielewa kwenye Bonde la Mto Msimbazi.
Katika eneo la Magomeni Suna, mwili wa mtu aliyetambuliwa kuwa ni Mwinyi Makame (20) ulikutwa pembeni mwa bonde la Msimbazi.Kenyela alisema maiti za watu wanne ambazo bado hazijatambuliwa na miili mingine imehifadhiwa katika hospitali ya Mwananyamala.
Alisema katika eneo hilo la Magomeni Suna, pia ulikutwa mwili wa mtu aliyetambuliwa kwa jina moja la Athuman umri (22) ambaye ni fundi magari na mwili huo pia umepelekwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
"Maiti zilizotambuliwa ni saba na ambazo hazikutambuliwa majina ni nane. Majeruhi wote walilazwa na kuruhusiwa,' alisema Waziri.
Katika eneo la Kigogo kwa Dua Said, Kamanda Kenyela alisema uliokotwa mwili wa mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka 12 ukiwa pembeni ya mto Msimbazi.Kamanda Kenyela alisema mwili wa Khalid Ali (22) ambaye ni mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Mgulani, ulikutwa ukielewa kwenye Bonde la Mto Msimbazi.
Katika eneo la Magomeni Suna, mwili wa mtu aliyetambuliwa kuwa ni Mwinyi Makame (20) ulikutwa pembeni mwa bonde la Msimbazi.Kenyela alisema maiti za watu wanne ambazo bado hazijatambuliwa na miili mingine imehifadhiwa katika hospitali ya Mwananyamala.
Alisema katika eneo hilo la Magomeni Suna, pia ulikutwa mwili wa mtu aliyetambuliwa kwa jina moja la Athuman umri (22) ambaye ni fundi magari na mwili huo pia umepelekwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Hosipitalini Dar
Kwa upande wake Ofisa Uhusiano Msaidizi wa Hospiali ya Muhimbili, Jeza Waziri alisema katika hospitali hiyo kulipokelewa maiti 15 na majeruhi 11.Waziri alisema kati ya maiti hao, wanawake ni watatu na wanaume 12. Alisema majeruhi saba kati ya hao 11 bado wamelazwa na kuendelea na matibabu hospitalini hapo."Maiti zilizotambuliwa ni saba na ambazo hazikutambuliwa majina ni nane. Majeruhi wote walilazwa na kuruhusiwa,' alisema Waziri.
Alitaja maiti waliotambuliwa kuwa ni Hidaya Amri (1) mkazi wa Jangwani, Hamisi Nyao (19) mkazi wa Vingunguti, Nyanda Kiangi (35)Mkazi wa Kigogo na mwingine aliyetambulika kwa jina la Bakari (10).
Wengine ni Nia Abrahamani (24) na Athumani (26) wote wakazi wa Magomeni.“Kuanzia jana (juzi) hadi saa 7.10 mchana leo (jana), tumepokea maiti 15 ikiwamo maiti moja ambayo inakuja sasa hivi ninavyozungumza na wewe,”alisema Waziri.
Katika hospitali ya Amana ambayo ipo katika Manispaa ya Ilala, kulikuwa na kifo cha mtu mmoja na majeruhi 45.
Dk Mwaluka Shanny wa hospitali hiyo, alisema kumekuwa na ongezeko la majeruhi kutoka 10 katika siku ya kwanza mpaka 45 jana.
Dk Shanny alisema wengi wa majeruhi hao wanatoka katika maeneo ya Kigogo na kwamba baadhi yao walipata mshituko na wengine majeraha madogo.
“Mpaka leo (jana) saa 8:00 kamili mchana, tumepokea majeruhi 45, kati yao yupo mwanamke mmoja (60) ambaye hali yake ni mbaya kutokana na kupata mshituko wa moyo,” alisema Dk Shaany.
Katika hospitali ya Temeke tangu mvua hizo zianze juzi, kuliripotiwa maiti moja na majeruhi wawili. Taarifa hizo zilitolewa jana na muuguzi wa zamu wa hospitali hiyo, Shamim Londo.
Wakati wenzao wa shule ya Mchikichini wakiwa wamenza kupata chakula, wao walisema hawajapata chakula wala maji licha ya viongozi kadhaa kuwatembelea.
“Viongozi wanakuja kutupa pole lakini sisi hatuhitaji pole ya mdomo tuna watoto wana njaa tangu jana hawakula chochote tunaomba msaada,” alisema Mwasa Samwel.Waathirika wengine walimuunga mkono mwenzao na kuongeza kuwa licha ya kukosa chakula pia hawana mashuka, vyandarua na nguo.
“Tumekuja kama tulivyo, tunaomba msaada, hatuna chakula hatuna nguo wala fedha vyote vimechukuliwa na mafuriko,” alisema Habiba Juma ambaye ana watoto wanne.
Wakati huohuo familia 15 zilizohifadhiwa katika Shule ya msingi Msimbazi baada ya nyumba zao kuzolewa na maji zimelalamikia kukosa misaada mbalimbali kikiwamo ya chakula.Fulugensi Kahima (37), mkazi wa Jangwani alisema msaada wa makazi waliopewa haitoshi na kwamba wanahitaji chakula hasa kwa watoto ambao ndio wamedhurika kwa kiasi kikubwa.
“Tumepewa hifadhi hapa lakini tangu tufike katika kituo hiki tumeishia kupewa juisi na maji lakini mpaka sasa hatujapata msaada wowote wa chakula zaidi ya kwenda kujitafutia wenyewe,” alisema Kahima.
Wengine ni Nia Abrahamani (24) na Athumani (26) wote wakazi wa Magomeni.“Kuanzia jana (juzi) hadi saa 7.10 mchana leo (jana), tumepokea maiti 15 ikiwamo maiti moja ambayo inakuja sasa hivi ninavyozungumza na wewe,”alisema Waziri.
Katika hospitali ya Amana ambayo ipo katika Manispaa ya Ilala, kulikuwa na kifo cha mtu mmoja na majeruhi 45.
Dk Mwaluka Shanny wa hospitali hiyo, alisema kumekuwa na ongezeko la majeruhi kutoka 10 katika siku ya kwanza mpaka 45 jana.
Dk Shanny alisema wengi wa majeruhi hao wanatoka katika maeneo ya Kigogo na kwamba baadhi yao walipata mshituko na wengine majeraha madogo.
“Mpaka leo (jana) saa 8:00 kamili mchana, tumepokea majeruhi 45, kati yao yupo mwanamke mmoja (60) ambaye hali yake ni mbaya kutokana na kupata mshituko wa moyo,” alisema Dk Shaany.
Katika hospitali ya Temeke tangu mvua hizo zianze juzi, kuliripotiwa maiti moja na majeruhi wawili. Taarifa hizo zilitolewa jana na muuguzi wa zamu wa hospitali hiyo, Shamim Londo.
Kambi za wathirika
Baadhi ya waathirika katika kambi ya Shule ya Msingi Gilman Rutihinda iliyoko Kigogo, wamelalamika kwamba tangu wafike kambini hapo juzi hawajapewa huduma yoyote, hata chakula.Wakati wenzao wa shule ya Mchikichini wakiwa wamenza kupata chakula, wao walisema hawajapata chakula wala maji licha ya viongozi kadhaa kuwatembelea.