CHAMELEON NI MINONGONI MWA WASANII BILIONEA AFRIKA


Anamiliki jumba la kifahari katika vilima vya Sekuku jijini Kampala, pia ana nyumba huko Arizona, Marekani, achilia ile ya Kigali, Rwanda aliyoinunua hivi karibuni kwa mamilioni ya shilingi. Ukiachilia mbali gari la kisasa aina ya Cadillac Escalade lililomgharimu zaidi ya Sh milioni 100, Chameleone ambaye ni baba wa watoto watu, pia anamiliki Mercedes Benz, BMW na aina nyingine za magari. 

Kwa ujumla, anakadiriwa kuwa na utajiri unaofikia Sh bilioni 1.5 kwa fedha za Tanzania. Na anasema bado anazisaka, kwani bila ya kuwa na tamaa ya kusaka mafanikio zaidi, ndoto huenda zisitimie.

Inasadikiwa kuwa, baada ya nyumba, magari na akaunti nono benki, sasa ana ndoto za kumiliki helikopta yake, baada ya kuwa amekuwa akikodi mara kadhaa ama kwenda katika matamasha au kama alivyofanya wakati anamuoa mkewe Daniela Atim.
 

Posted by Bigie on 10:26 PM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.