MZEE YUSUF AIBIWA VIATU VYAKE AKIWA NDANI YA STUDIO MKOANI IRINGA
JAMII 5:58 PM
Mzee Yusuph akionyesha show la ukweli katika ukumbi wa Highland mjini Iringa usiku huu
Vyanzo vya ndani viliudokeza mtandao huu wa kuwa mzee Yusuph aliibiwa majira ya saa 12 za jioni wakati akiwa ndani ya studio za radio hiyo akifanyiwa mahojiano ya moja kwa moja juu ya show yake mjini Iringa
Hata hivyo mpasha habari wetu alisema kuwa wakati msanii huyo akiingia katika studi hizo alilazimika kuvua viatu vyake na kuviacha sehemu ya mapokezi ya kituo hicho cha radio kama kawaida kabla ya kuingia studio kufanya mahojiano ila alipotoka nje baada ya kumaliza kipindi ili aweze kuwahi kujiandaa kwa ajili ya kwenda ukumbini ghafla hakuweza kuona viatu vyake kabla ya kuazimwa viatu kwa muda ili aweze kutoa eneo hilo.
Hata hivyo utata juu ya wizi huo wa viatu vya msanii huyo bado umetanda baada ya baadhi ya wa watu kumshuku mmoja kati ya watangazaji kuwa amefanya wizi huo huku baadhi yao wakidai yawezekana ni vibaka walifika katika kituo hicho na kuiba viatu hivyo .
Akizungumza mara baada ya kutoa burudani kwa wakazi wa mji wa Iringa ndani ya ya Ukumbi wa Highland mjini Iringa mzee Yusuph alisema kuwa kamwe katika maisha yake hataweza kusahau tukio hilo la aibu ambalo limemkuta mjini Iringa ndani ya kituo hicho cha radio.
'Kwa kweli napenda kuwapongeza wadau wangu kwakujitokeza kwa wingi na kuendelea kupenda kazi zangu .....ila katika maisha yangu kamwe sitasahau mkoa wa Iringa ....kweli ni vigumu kuamini ila yametokea mwenzenu leo nimeibiwa viatu tena nikiwa sehemu nyeti sana ila ni siri yangu sitaki kutaja sehemu hiyo ila nimeibiwa viatu vyangu nilivyovipenda sana"alisema mzee Yusuph na kwenda kukaa katika kiti.
Kutokana na tukio hilo la kuibiwa viatu mzee Yusuph alichelewa kupanda jukwaani na kupanda majira ya saa 6.45 usiku huku akionekana ni mtu wa kulazimisha furaha japo huzuni ndio ilichukuwa nafasi kubwa katika show yake hiyo mjini Iringa.
Hata hivyo baadhi ya mashabiki waliomba kumchangia fedha ili kununua kiatu hicho japo mpango huo haukuzaaa matunda kutokana na muda.
Show hiyo ya mzee Yusuph na kundi lake mjini Iringa imeweza kufana japo ni show iliyofanyika jumapili kinyume na wengi walivyofikiri kuwa yawezekana show hiyo ikakosa watu.
