DR.KIKWETE AREJEA NCHINI
JAMII 6:37 PM
Rais Jakaya Kikwete akiwa katika mazungumzo na Makamu wa Rais Dr Mohamed Ghalib Bilal na Waziri Mkuu Mh Mizengo Pinda mara baada ya kurejea jijjini Dar es salaam kutoka Kampala, Uganda, alikohudhuria mkutano wa siku mbili wa wakuu wa nchi za maziwa makuu
Rais Jakaya Kikwete akiagwa na Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Uganda, Mh Nsavike G. Ndatta katika uwanja wa ndege wa Entebbe Desemba 17, 2011 wakati akiondoka Uganda kurejea nyumbani baada ya kuhudhuria mkutano wa siku mbili wa wakuu wa nchi za maziwa makuu
Rais Jakaya Kikwete akiwakabidhi Bw. Clement A. Chagula na bintiye Olivia A. Chagula medali kwa niaba ya baba na babu yao Marehemu Dkt. Wilbert Chagula, ambaye alikuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam wa kwanza mzalendo na mmoja wa mawaziri katika serikali ya awamu ya kwanza ni mmoja wa watu maarufu waliotunukiwa nishani katika kuadhimisha miaka 50 ya Uhuru. Bw Chagula, ambaye ni mtoto wa marehemu, hakuweza kufika Dar es salaam kupokea medali hiyo na Rais alipokuwa Kampala akatumia nafasi hiyo kumpatia katika hoteli ya Speke Commonwealth Resort.