JACK PATRICK AFUNGA NDOA HUKU "MASINGAMANGO","UMALAYA" NA HISTORIA YA NYUMA VIKIMTOA MACHOZI
JAMII 10:29 PM
Mwanamitindo mwenye jina kubwa Bongo, Jacqueline Patrick, ameolewa na mtoto wa aliyekuwa mwanasiasa maarufu nchini, Chifu Abdallah Fundikira, Abdullatif Fundikira.
Kwa upande mwingine wa shilingi, ndoa hiyo imemtoa chozi Jack kwa kile alichodai kwamba ameshinda changamoto nyingi mpaka kufikia kuitwa mke wa Abdulatif.
Baada ya kufunga ndoa, iliyofungishwa na mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Hatibu Bernard, katika Ufukwe wa Hoteli ya Coral, Masaki, Dar es Salaam, Jumamosi iliyopita, Jack alisema:
Kwa upande mwingine wa shilingi, ndoa hiyo imemtoa chozi Jack kwa kile alichodai kwamba ameshinda changamoto nyingi mpaka kufikia kuitwa mke wa Abdulatif.
Baada ya kufunga ndoa, iliyofungishwa na mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Hatibu Bernard, katika Ufukwe wa Hoteli ya Coral, Masaki, Dar es Salaam, Jumamosi iliyopita, Jack alisema:
“Kuna watu walinisema sana, waliniita malaya, wakasema siwezi kuolewa na wala sifai kuwa mke wa mtu. Hayo maneno yaliniuma sana na yananitoa machozi leo baada ya kuolewa.
“Nawaahidi Watanzania kwamba nitaidumisha ndoa yangu, sijaolewa na Abdullatif kwa bahati mbaya, nampenda sana na ahadi yangu kwake ni kwamba nitakuwa mke bora na mama bora wa familia.”
Jack aliwapiga dongo wote aliowahi kushea nao penzi kwa maelezo kuwa imebaki historia na sasa anaangalia maisha yake mapya na mume wake.
“Nitakuwa mwaminifu kwenye ndoa yangu. Wote ambao nimewahi kuwa nao, walikuwa wananiandaa kuja kuishi vizuri na mume wangu Abdullatif,” alisema Jack.
Ndoa ya Jack na Abdul, ilikusanya familia zote mbili na baada ya mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni kuifungisha, sherehe zilihamia kwenye Ukumbi wa Kili Marque, uliopo ndani ya Hoteli ya Hyatt Regency Dar es Salaam, The Kilimanjaro (zamani Kilimanjaro Kempinski)
Katika ukumbi huo, kulikuwa na mambo mengi ya kuvutia lakini kubwa ni jinsi mastaa mbalimbali walivyompa ushirikiano kwa kujitokeza kusherehekea naye tukio hilo muhimu.
Mastaa walioinogesha sherehe ni Christine John ‘Sintah’, Jacqueline Wolper, Aunt Ezekiel, Lisa Jensen, Mboni Masimba, Ambwene Yesaya ‘AY’, Belina Mgeni na wengine wengi.
Ndoa hiyo, ilipambwa pia na wanamitindo mbalimbali ambao waliingia kucheza muziki wa Kwaito na baadaye Sebene, wakipamba shoo ya kuwakaribisha maharusi ukumbini.



