MFANYABIASHARA AFIA HOTELINI AKIWA NA KETE 60 ZA MADAWA YA KULEVYA


Kete 60 za madawa ya kulevya zimekutwa mwilini mwa Bushaga Masalai mwenye umri wa miaka 30, mkazi wa jijini Dar es Salaam ambaye ni mfanyabiashara kati ya Dar es Salaam na Tunduma mkoani Mbeya .Mfanya biashara huyo amefariki dunia akiwa chumba cha kupanga katika Hoteli ya High Class, Tunduma.

Marehemu alifika hotelini hapo Desemba 2, mwaka huu akitokea jijini Dar Es Salaam, lakini Desemba 3, wahudumu walipokuwa katika shughuli zao za usafi katika hoteli hiyo walijaribu kugonga mlango wa chumba hicho alichopanga marehemu, lakini haukufunguliwa kutokana na ukimya huo waliamua kwenda kutoa taarifa kituo cha polisi majira ya saa 6 mchana.

 Jeshi la polisi mji mdogo wa Tunduma baada ya kupewa taarifa lilifika hotelini majira ya saa 6 na dakika 30 ili kufanya uchunguzi na kisha kuubomboa mlango huo ndipo walipomkuta Bwana Bushanga akiwa amefariki dunia.
  Kete hizo zitasafirishwa kwa mkemia mkuu jijini Dar es salaam kwa ajili ya uchunguzi ili kubaini aina gani ya madawa hayo, pamoja na thamani yake na kwamba shughuli za kusafirisha mwili wa marehemu zitafanyika baada ka kukamilika kwa zoezi la kuwapata ndugu wa marehemu huyo.

Posted by Bigie on 7:24 PM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.