KIJANA MWINGINE AUAWA KIKATILI MKOANI MBEYA...APIGWA NA KUCHOMWA MOTO

Utaratibu wa kujichukulia Sheria mikononi inaendelea kutawala hususan katika Mkoa wa Mbeya. 
 
Pichani baadhi ya wakazi wa mtaa wa Mwanyanje, Kata ya Igawilo mkoani Mbeya wakiwa na nyuso za huzuni baada ya mwananchi mmoja ambaye jina lake halikufahamika mara moja kupigwa na kisha kuchomwa moto ambao uliteketeza mwili wake.
 
Mtu huyo alituhumiwa kuwa ni mwizi licha ya kutofahamika alichoiba au aliyeibiwa kijijini hapo. 
 
Ukatiri usio kifani unaonekana dhahiri katika Picha hii ambapo watu wasio kuwa na huruma waliamua kujichukulia Sheria mikononi kwa kumpiga kisha kumchoma moto kama inavyoonekana.
 
Pichani watoto wa Kata ya Igawilo mkoani Mbeya wakiangalia kwa nyuso za huzuni baada ya mwananchi mmoja ambaye jina lake halikufahamika mara moja kuchomwa moto na kuuteketeza mwili wake. Mtu huyo alituhumiwa kuwa ni mwizi licha ya kutofahamika alichoiba au aliyeibiwa kijijini hapo.

Posted by Bigie on 2:16 AM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.