KUNDI LA "WELAWELA" LAMLIZA BI HARUS MTARAJIWA BAADA YA KUTUMBUIZA KWA STAILI YA "TENDO LA NDOA"


AMA kweli dunia uwanja wa fujo! Biharusi mtarajiwa mjini hapa, Sofia Majid amejikuta akiangua kilio baada ya kundi la wasichana watatu la jijini Dar es Salaam almaarufu Welawela kumwaga radhi kwenye sherehe ya ‘kitchen party’ yake.

Tukio hilo lililoshuhudiwa na Mpekuzi wetu  lilijiri kwenye Ukumbi wa Nashera mjini hapa hivi karibuni mbele ya Mbunge wa Viti Maalum Vijana CCM, Mkoa wa Arusha Mhe. Catherine Magige.

Welawela, wakiwa na mwimbaji wa taarabu aliyealikwa kutumbuiza, Afua Suleiman walipopewa nafasi ya kutumbuiza na ‘emsii’ wa shughuli hiyo, Hawa Chamng’anda walivamia kitanda cha zawadi cha biharusi na kuanza kucheza Makhirikhiri kwa kugaragazana kwa staili ya tendo la ndoa na kukiacha kitanda hicho kikiwa hakitamaniki kwa kukifinyanga.


Kitendo hicho, pamoja na burudani waliyoitoa vilimfanya biharusi kushindwa kujizuia na kuangua kilio

Posted by Bigie on 11:08 PM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.