SAFARI YA KUUPELEKA MWENGE WA UHURU KATIKA KILELE CHA MLIMA KILIMANJARO YAANZA


Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe.Leonidas Gama akimpa mkono wa kumtakia heri mmoja wa vijana wanaopandisha Mwenge wa Uhuru kwenye kilele cha Mlima Kilimanjaro kwenye hifadhi ya Mlima Kilimanjaro zilizoko Marangu Mkoani Kilimanjaro jana  tarehe 5.12.2011.
Vijana wanaopandisha Mwenge wa Uhuru kwenye kilele cha Mlima Kilimanjaro wanaonekana wakianza safari yao kwenye hifadhi ya Mlima Kilimanjaro Marangu Mkoani Kilimanjaro jana  tarehe 5.12.2011.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Leonidas Gama pamoja na Viongozi wa Mkaoa wa Kilimanjaro na wawakilishi wa Wizara ya Habari ,Vijana ,Utamaduni na Michezo wakiwasindikizaVijana wanaopandisha Mwenge wa Uhuru kwenye Kilele cha Mlima Kilimanjaro tayari kwa safari jana Marangu kwenye Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro Mkoani Kilimanjaro.
Vijana wanaopandisha Mwenge wa Uhuru kwenye kilele cha Mlima Kilimanjaro walioagwa rasmi na  Mhe.Rais Jakaya Mrisho Kikwete  Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam hivi karibuni  wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Leonidas T. Gama akiwaaga kwenye shughuli fupi iliyofanyika  Marangu kwenye Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA)  Mkoani Kilimanjaro jana  tarehe 5.12.2011
Vijana wanaopandisha Mwenge wa Uhuru kwenye kilele cha Mlima Kilimanjaro wakiwa tayari kwa kuanzakupandisha mlima huo na Mwenge.

Posted by Bigie on 4:57 PM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.