LULU AMRUDIA MWENYEZI MUNGU...

BAADA ya kufanya jitihada za hapa na pale za kujisafisha kufuatia kuandamwa na msururu wa skendo, Elizabeth Michael ‘Lulu’,  ameamua kumgeukia Mungu
Staa huyo mkali wa muvi za Kibongo na video za wanamuziki wa Kizazi Kipya, anakiri kutenda dhambi nyingi pamoja na umri wake mdogo wa miaka 18 hivyo kuhitaji utakaso kutoka kwa Mungu.

Akizungumza na Mpekuzi wetu  mwanzoni mwa wiki hii, Lulu alisema kwa sasa anatembea na Biblia ikiwa ni sehemu ya kutambua uwepo wa Mungu kila sehemu anapokwenda.

Lulu alisema kuna siku alikaa na rafiki yake, akamwambia kuwa hivi sasa dunia imeharibika na kila wanachokifanya (maovu) ni marudio tu kwani kuna watu walishafanya uozo, lakini hawapo duniani.

Lulu aliweka kweupe kuwa tangu siku hiyo, aliamua kujiweka karibu na Mungu hivyo akatafuta kitabu hicho kitakatifu ili ajifunze Neno la Mungu kiundani ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kwenda mbinguni.
Lulu anayesali Kanisa Katoliki Parokia ya Kristo Mfalme Tabata, Dar es Salaam alifunguka:
“Sasa hivi popote ninapokwenda lazima niwe na Biblia. Hata katika kitanda ninacholala, ukibinua mto utakutana nayo.
“Ukweli ni kwamba katika kila ninachofanya ni lazima nisali kwanza.

“Katika maisha tunayoishi na siku tulizonazo ni za uovu uliopindukia, nimegundua ni vyema kila ulipo uwe na utukufu wa Mungu kwa sababu hakuna anayejua siku wala saa ya kuondoka hapa duniani hivyo nawasihi watu wote kumjua Mungu,”
Lulu.

Kama Lulu amejitambua na kuamua kumrudia Mungu ni jambo zuri na anastahili pongezi, lakini tahadhari ni kwamba anapaswa kushikilia aina hiyo ya maisha na siyo baada ya siku mbili tusikie karudi tena kulekule.

Posted by Bigie on 7:24 PM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.