UVUTAJI WA SIGARA KUPITA KIASI PAMOJA NA POMBE ZITAMPONZA NISHA...
JAMII 7:45 PM
MSANII wa filamu mwenye mvuto wa aina yake, Salma Jabu ‘Nisha’ anadaiwa kukubuhu katika uvutaji wa sigara na unywaji wa pombe kupita kiasi, tabia inayomfanya awe katika wakati mgumu.
Mpekuzi wetu juzikati alimnasa Nisha kwenye Mgahawa wa Rose Garden uliopo Mikocheni jijini Dar akivuta fegi huku akiwa ‘tungi’ na alipomhoji sababu ya kuwa vile aliishia kuongea maneno yasiyoeleweka.
Aidha, mrembo aliyekuwa ‘beneti’ na Nisha , alimnong’oneza mpekuzi wetu juu ya hali ya msanii huyo kwa kusema:
“Huyu bwana asipoangalia pombe na sigara vitamuua, hapo unapomuona anadai mpenzi wake kamzingua kwa hiyo anaona bora alewe ili kuondoa mawazo, mimi mwenyewe namuonea huruma.”
Hata hivyo, dakika chache baadaye staa huyo wa Filamu ya Obsession akiwa na shoga yake waliingia kwenye gari lake na kutimua zao kukwepa usumbufu wa mpekuzi wetu

