MAINDA AWEKA WAZI KUWA YEYE SI WAKALA WA "MITANDAO" KWA WANAUME

HUKU kukiwa na madai kwamba wasichana wanaovaa mikufu miguuni ‘vikuku’ wanajihusisha na tabia mbaya ya kufanya mapenzi kinyume na maumbile, msanii wa filamu Bongo, Ruth Suka ‘ Mainda’ amefunguka na kueleza kuwa, yeye ni tofauti kwani anavaa kama urembo tu.

Akiongea na Mpekuzi wetu  juzi baada ya kunaswa akiwa amevaa urembo huo, Mainda alisema amekuwa akisikia maneno hayo lakini yeye haamini ila anachojua ni urembo kama ilivyo kwa wale wanaovaa cheni kiunoni na shingoni.

Alisema wanaofikia hatua ya kudhani wanaovaa urembo huo miguuni wanajihusisha na tabia mbaya ya kugawa ‘mtandao’ kwa wanaume, wanakosea na si jambo la busara kuendelea kuwa na fikira hizo potofu.

 “Kuvaa kwangu cheni mguuni hakumaanishi chochote, hii ni moja ya urembo tu, ukifuatilia kuna wanaovaa cheni kiunoni na shingoni, mimi nimeamua kuvaa mguuni kuna tatizo gani? Wanaofikiria tofauti wana uelewa mdogo wa mambo,” alisema Mainda.

Katika siku za hivi karibuni kumekuwa na hisia tofauti juu ya wanawake wanaovaa vikuku lakini wanapoulizwa huishia kusema ni urembo tu.

Posted by Bigie on 8:26 PM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.