JOSEPH KABILA ASHINDA URAIS TENA

RAIS Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), amefanikiwa kutetea kiti chake katika uchaguzi  uliofanyika wiki iliyopita, akiwa amejikusanyia kura 8,880,994 (sawa na asilimia 49), akimuacha mpinzani wake mkuu, Etienne Tshisekedi, aliyeambulia kura 5,864,755 (sawa na asilimia 32).

Katika uchaguzi huo wa pili wa kidemokrasia tangu kumalizika kwa vita ya wenyewe kwa wenyewe nchini humo, wagombea 10 walichuana katika nafasi ya urais, ambapo baadhi yao akiwamo Tshisekedi, wameyapinga matokeo hayo wakidai kulikuwa na hila za kumuwezesha Kabila kushinda.

Baada ya kutangazwa kwa matokeo hayo, kumekuwa na matukio ya vurugu katika baadhi ya maeneo ya mji mkuu wa Kinshasa, ambayo yameweza kutulizwa na askari waliotanda barabarani.

Katika eneo la Jiji la Goma, watu wameonekana wakipita wakishangilia ushindi wa Kabila kuongoza tena taifa hilo tangu kufariki dunia kwa baba yake, Laurent Kabila mwaka 2001.

Posted by Bigie on 8:48 PM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.