MAJAJI TOKA TANZANIA WASHINDA UCHAGUZI WA UMOJA WA MATAIFA
JAMII 8:23 PM
Jaji William Hussein Sekule ambaye pamoja na Jaji Joseph Chiondo Masanche wote kutoka Tanzania wameingia katika orodha ya majaji wa Mfumo mpya wa Kimataifa wa kushughulikia kesi za Mashauri ya Masalia ya Mahakama za Makosa ya Jinai ( International Residual Mechanism for Criminal Tribunals).
Majaji hao wameingia katika orodha hiyo wakiwa ni sehemu ya majaji 25 walioshinda baada ya kupingiwa kura ya siri kati ya majaji 36 walioomba nafasi hiyo.
Upigaji kura huo ulifanywa na Baraza Kuu la 66 la Umoja wa Mataifa na umekamilika siku ya Jumanne