MAKAHABA WAOKOKA......
JAMII 6:42 AM
BAADHI ya akina dadapoa wanaofanya biashara ya kuuza miili yao katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar, wamemgeukia Mungu kwa ridhaa yao ndani ya Kanisa la Huduma ya Maombezi, Mbezi linaloongozwa na Nabii Frola Peter.
Tukio hilo lililojiri kanisani hapo Desemba 18, mwaka huu baada ya mkuu wa kanisa hilo, Nabii Flora (pichani) aliendesha maombi ya kuwarudisha akina dada hao kwa bwana kwa kuwa ni kondoo waliopotea.
Akizungumza baada ya kuwa ‘mpya’ mmoja wa makahaba hao aliyejitambulisha kwa jina moja la Ester (22), mkazi wa Mwananyamala, Dar alisema:
“Nilianza ukahaba baada ya kuhitimu kidato cha nne mwaka 2008 katika Shule ya Sekondari Msaki Memorial Girls ya jijini Dar es Salaam.
“Nilikuwa napata pesa nyingi, nilianza kuwa jeuri nyumbani nikiamini maisha bora yanapatikana kutokana na biashara ya kuuza mwili, kumbe nilikuwa namkosea Mungu,” alisema Ester.
Akasema pamoja na kuwa na umri mdogo, lakini wateja wake wakubwa walikuwa ‘wababa’ wenye shughuli za maana.
Katika hali ya kushangaza, Ester alisema katika kipindi chote cha ukahaba, alishatoa mimba saba kwa sababu kupata mtoto kwa wakati huo kungemharibia biashara yake.
Mbali na dada huyo, kahaba mwingine aliyekata shauri siku hiyo ni Somoye alisema alikutana na Ester katika ‘kazi’, wakawa marafiki, alichopitia Ester ndicho alichokipitia yeye.
Kwa mujibu wa Nabii Flora, mabinti hao watabadilika na kupata kazi zenye maadili mazuri muda si mrefu