DIAMOND AFUNGUKA NA KUDAI KUWA HAWEZI KUACHANA NA WEMA SEPETU
JAMII 6:31 AM
UCHUMBA wa staa wa muziki wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul Jumaa ‘Diamond’ na Miss Tanzania 2006/07, Wema Isaac Sepetu, umekucha tena licha ya shutuma za Wema kwa mlimbwende Jokate Mwegelo kwamba alimkuta akiwa ‘kihasarahasara’ na mpenzi wake huyo.
.
Hata hivyo, mara baada ya madai ya Wema, Desemba 10, mwaka huu, Diamond alipanda ndege kwenda London, Uingereza kwa mkataba wa kutumbuiza shoo kadhaa.
Akihojiwa kwa dakika 30 na mtangazaji Miss Justina George katika Live Talk Show ya AILTV nchini humo, nyota huyo alishindwa kuweka wazi kwamba, alitoka Bongo akiwa ametuhumiwa kusaliti, badala yake akasema ana mchumba (Wema) ambaye anampenda kupita maelezo.
Akizungumza na MPEKUZI wetu kwa njia ya simu akiwa London Desemba 16, mwaka huu, Diamond alisema baada ya kumaliza shoo zake nchini humo angerejea Bongo na bonge la ‘sapraizi’ kwa Wema.
Alipoambiwa huku Bongo, Wema amekuwa akitangaza kummwaga baada ya kudaiwa kukutwa sirini na Jokate, Diamond alijibu:
“Hakuna kuachana hapa, Wema bado ni mchumba wangu, nampenda sana.”