MASHINDANO YA SHIMIVUTA YAMALIZIKA MJINI MOROGORO HUKU CBE WAKINYAKUA VIKOMBE...

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro, Amir Nondo ( kushoto) akimkabidhi Nahodha wa timu ya Mpira wa Miguu ya Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE),Benedict Masasi ( kulia) kikombe cha Ubingwa wa soka cha mashindano ya 36 ya Shirikisho la Michezo la Vyuo vya Elimu ya Juu Tanzania (SHIMIVUTA),yaliyoanza Desemba 9 na kufikia kilele Desemba 18, mwaka huu, Mkoani ( katikati ) ni Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Dk Zakaria Mganirwa, timu hiyo iliishinda LGTI bao 5-0.

WASHINDI WA PILI SOKA TIMU YA CHUO CHA SERIKALI ZA MITAA (LGTI)  AKIKABIDHIWA KIKOMBE NA MEYA AMIR NONDO.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro, Amir Nondo ( kushoto) akimkabidhi Nahodha wa timu ya Mpira wa Netiboli wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE)Evodia Sanga ( kulia) kikombe cha Ubingwa wa Netiboli cha mashindano ya 36 ya Shirikisho la Michezo la Vyuo vya Elimu ya Juu Tanzania (SHIMIVUTA),yaliyoanza Desemba 9 na kufikia kilele Desemba 18, mwaka huu, Mkoani ( katikati ) ni Mkuu wa Chuo cha Taifa Cha Usafilishaji (NIT), Dk Zakaria Mganirwa, CBE iliifunga LGTI mabao 38-30.
Baadhi ya Wachezaji Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) wa timu mbalimbali wakishangilia kwa pamoja ushindi walioupata wa timu zao za soka, netiboli na Basketiboli kunyakua vikombe vya ubingwa wa michezo hiyo katika mashindano ya 36 ya Shirikisho la Michezo la Vyuo vya Elimu ya Juu Tanzania ( SHIMIVUTA), yaliyoanza Desemba 9 na kufikia kilele Desemba 18, mwaka huu, Mkoani Morogoro.
WACHEAJI WA TIMU YA LGTI (KUSHOTO) NA CBE KULIA NA WAAMUZI WAO KABLA YA MCHEZO WA FAINALI NETIBOLI.
Mwalimu wa timu ya soka la Chuo cha Serikali za Mitaa (LGTI) akitoa maelekezo wakati wa mapinziko,baada ya kuwa nyumba kwa mabao 2-0 dhidi ya timu ya CBE, hata hivyo hadi dakika tisini za mchezo huo unamalizika, CBE waliobuka kidedea kwa kupata ushindi mnono wa mabao 5-0 na kutwaa kikombe cha Ubingwa wa michezo ya 36 ya Shimivuta.

Posted by Bigie on 11:14 PM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.